Jamii FM

Naliendele Mtwara wamlilia Hayati Magufuli

23 March 2021, 18:05 pm

Wananchi wa kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara Mikindani wametoa salamu za pole kwa Watanzani kufuatia  kifo cha Rais Dkt.John Pombe Magufuli kilichotangazwa usiku wa kuamkia leo Machi 18,2021.

Kata ya Naliendele

Wakizungumza kwa masikitiko makubwa wameeleza namna ambavyo watamkumbuka Rais Dkt.Magufuli kwa mazuri mengi aliyoyafanya ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara za kusini pamoja na uboreshwaji wa Bandari ya Mtwara.

Aidha Wananchi hao wamesema kuwa watamkumbuka Dkt.John Pombe Magufuli kwa uzalendo aliounesha kwa Watanzania kwa kujali wanyonge, kutoa huduma ya elimu bure, na mengine mengi.

Sauti za Wananchi wa Kata ya Naliendele wamlilia Hayati Rais Magufuri

Taarifa ya kifo cha Rais Magufuli ilitolewa na Makamu  wa rais kwa wakati huo ambapo sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kilichotokea hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.