Jamii FM

Athari ya mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri upatikanaji wa samaki

19 March 2024, 15:55 pm

wachuuzi wa samaki wakiwa kwenye mnada. Picha na Musa Mtepa

“Ongezeko la joto Baharini na  uwingi wa maji ya mvua kutoka Kwenye mito mbalimbali kumechangia kwa kiasi kikubwa  kupungua upatikanaji wa Samaki “

Na Musa Mtepa

Baadhi ya Wavuvi wa  wanaofanya shughuli za uvuvi katika ukanda  wa Bahari na Pwani ya Mkoa  wa Mtwara  wameelezea  changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi inavyo waathiri katika upatikanaji wa Samaki  na hali yao ya kiuchumi.

Wakizungumza na Jamii Fm Radio March 18,2024 Wavuvi hao wamesema kuwa ongezeko la joto Baharini na  uwingi wa maji ya mvua kutoka Kwenye mito mbalimbali kumechangia kwa kiasi kikubwa  kupungua upatikanaji wa Samaki .

Sauti ya wavuvi wa Samaki

Saidi Dadi ni mkazi wa mtaa wa Magomeni Manispaa ya Mtwara ambae pia ni mvuvi  samaki  kwa zaidi ya miaka 30 amesema  zamani Samaki walikuwa hawapatikani umbali mrefu ukilinganisha na sasa hivi  ambapo huwalazimu  kwenda umbali mrefu kuwapata.

Sauti ya Saidi Dadi mvuvi wa samaki

Naye Sheha Shante  Mwenyekiti wa Wavuvi  Manispaa ya Mtwara Mikindani amesema kutokana na upatikanji wa kuwa mchache imepelekea maisha ya Wavuvi kuwa magumu kiuchumi  huku akiiomba serikali kuwaangali kwa jicho la kwa kuwapatia mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya Sheha Shante Mwenyekiti wa Wavuvi Manispaa ya Mtwara Mikindani

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  mtandao Wilaya utunzaji wa Mazingira ya Pwani na Bahari (BMU) Shabani Mayonzi  amesema ili kurejesha katika hali yake ya asili ya Bahari lazima Serikali na Wadau mbalimbali  kuwekeza katika utoaji wa elimu juu ya utunzaji wa mazingira ya Bahari ikiwemo upandaji wa mikoko pamoja na ulimaji wa zao la Mwani.

Sauti ya Mwenyekiti wa  mtandao Wilaya utunzaji wa Mazingira ya Pwani na Bahari (BMU) Shabani Mayonzi