Wafanyakazi wa TAKUKURU wakiwa ndani ya studio za Jamii FM
Jamii FM

TAKUKURU Mtwara: Tunawashukuru Waandishi wa Habari na Wadau

28 June 2022, 20:46 pm

Taasisi ya  Kupambana na Kuzuia Rushwa  (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara imewashukuru wananchi na taasisi mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari kwa namna ambavyo wametoa ushirikiano katika kuelimisha umma kwa  mwaka wa fedha  unaoishia Juni 30, 2022 huku TAKUKURU ikifikia malengo yake ya kutoa huduma kwa wananchi katika nyanja mbalimbali ya  Elimu,  na kushughulikia malalamiko mbalimbali kutoka kwa wanachi.

pichani ni wafanyakazi wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara na wafanyakazi wa Jamii FM

pichani ni wafanyakazi wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara na wafanyakazi wa Jamii FM wakiwa katika picha ya pamoja

Wakizungumza na Jamii FM leo juni 28, 2022 Mkuu wa Dawati la Huduma kwa Umma Ndugu Paschal Mhagama amesema “Zipo taasisi nyingi tumeshirikiana nazo katika michakato mbalimbali ya kuhakikisha tunazuia na kupambana na rushwa, kwahiyo tunawashukuru wote kiujumla, kwa kiwango kikubwa, ufikiwaji wetu wa malengo ni kwasababu ya ushirikiano huo”

Wafanyakazi wa TAKUKURU wakiwa ndani ya studio za Jamii FM

 

Katika mazungumzo hayo, TAKUKURU Mkoa wa Mtwara imesema, katika mwaka wa fedha ujao wanahitaji kuendelea kushirikiana na wananchi pamoja na wadau ili kuendelea kutoa ushirikiano ili kuleta mabadiriko ya kitabia katika jamii  ili kupunguza kabisa suala la rushwa.

Nae Mkuu wa Dawati la Uchunguzi Ndugu Alex Myamba amesema “ watoa taarifa ni watu ambao wapo kwenye jamii ambao wanakutana na changamoto mbalimbali za rushwa, na waandishi wa habari katika kazi zenu ndio mnaibua maovu mbalimbali ambayo yanatusaidia hata sisi kuyafanyia kazi”

Sikiliza mahojiano hapo chini: https://radiotadio.co.tz/jamiifm/wp-content/uploads/sites/4/2022/06/takukuru-20220628-090000.mp3