Jamii FM

Bibi Esha apata makazi Mapya

16 March 2021, 08:02 am

Jamii fm radio kwa kushirikiana na Wanasalam kanda ya kusini yaani Mikoa ya Mtwara na Lindi pamoja na wadau wengine wamefanikiwa kujenga nyumba katika eneo la Mtaa wa Namayanga Kata ya Mtawanya Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa ajili ya Bibi Esha Bint Ally ambaye alikuwa akiishi maisha magumu.

Ujenzi huo umekamilika siku ya tarehe 13.03.2021 na hivyo kumkabidhi Nyumba yake, Haya ndio makazi mapya ya Bibi Esha

Kwa mara ya kwanza Jamii fm Radio kupitia kipindi cha Dira ya asubuhi iliibua story inayomhusu Bibi huyo ambaye alikuwa akiishi kwenye banda lilikuwa likifugiwa kuku ambalo baada alisaidiwa na wasamalia wema.

kwa miaka miwili mfululizo ameishi humo pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa zaidi ya miaka 40 ambaye ni mlemavu wa akili na ni bubu hivyo kumnyima bibi haki ya faragha muda wote awapo kwenye banda hilo.

Makazi ya awali ya Bibi Esha

Baada ya taarifa hiyo kutoka Jamii fm iliunda kamati ndoto ya kusimamia michango, kamati iliyotokana na wanasalam hivyo kufanikisha kukusanya kiasi cha pesa ambacho kilisaidia kununua Vifaa vya ujenzi huku nguvu kazi ya wasikilizaji wa radio ikiwa imetumika kwa asilimia mia moja.

Akiongea na Jamii fm radio Mjukuu wa pekee wa Bibi huyo anayeitwa Subira Abduli ameishukuru sana Jamii fm radio na kutaka iwe mfano wa kuigwa kwa kuwa imekuwa ni Radio inayowasaidia wanyonge, na hata kuwafariji maana kwa sasa Bibi yake ataishi maisha ya furaha na amani.

Picha ya pamoja ya wadau na waandishi wa Jamiifm iliyopigwa mbele ya nyumba hiyo baada ya kukamilika kea ujenzi.

Hii ni Nyumba ya pili kujengwa na Jamii fm radio kwa kushirikiana na wadau mbalimbali Ikiwa ya kwanza ilijengwa mwaka 2019 katika Kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara Mikindani, Hali inayopelekea kudumisha umoja Kati ya kituo na wanajamii.