Jamii FM

Wananchi wa Mtiniko waipongeza serikali kwa kupata nishati ya umeme

5 February 2021, 07:44 am

Wananchi wa kijiji cha Mtiniko Halmashauri ya mji Nanyamba mkoani mtwara wameipongeza serikali kwa kuwapelekea huduma ya umeme wa REA na kusema uwepo wa umeme huo umesaidia kuinua kipato cha wakazi hao kwa kuwepo kwa viwanda vidogovidogo mitaani. Akiongea na Jamii fm radio mwenyekiti wa kijiji hicho Ndugu Hamisi Ling’wenye amewataka wananchi wake kuendelea kuitumia fursa ya uwepo wa umeme huo kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.