Jamii FM

Waandishi wa Habari wanawake Mtwara waadhimisha IWD21

8 March 2021, 09:52 am

Waandishi wa Habari Wanawake kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Mtwara (MTPC) Leo Machi 8, 2021 wameadhimisha siku ya Wanawake Duniani katika shule ya sekondari ya Mtwara Sisters.

Waandishi wa Habari Wanawake na Mdau kutoka PBZ Bank wakimkabidhi mwakilishi wa wanafunzi hao shuleni kwao

Akizungumza katika maadhimisho hayo mwenyekiti wa MTPC Grace Kasembe amesema wameona vyema kushiriki na wanafunzi hao ili kuwatia Moyo katika msomo pia ili kuwajenga kisaikolojia maana ni viongozi wajao.

Wanafunzi na waandishi wa Habari Wanawake wa Mkoani Mtwara katika picha ya pamoja

Mratibu wa Chama hicho Mwajuma Kitwana amewashukuru wadau walioshirikiana nao katika kuadhimisha siku hii pia amewaasa wanafunzi hao kuthamini pesa inayotolewa na wazazi wao na kuwekeza kwenye Elimu wanayoipata sasa maana ndio msingi wa maisha.

Wanafunzi wameonyesha nyuso za furaha kuonyesha namna walivyofurahi kukutana na waandishi hao ambao wamekuwa vioo katika Jamii.

Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaandhimishwa Kimkoa mkoani Mtwara ambapo kauli mbiu ni “wanawake katika uongozi, chachu kufikia Dunia yenye usawa