Jamii FM

Kipindi: Fahamu ulemavu aina ya mguu kifundo au unyayo uliopinda

3 June 2023, 14:50 pm

Siku ya mguu kifundo au unyayo uliopinda inaadhimishwa leo Juni 3, 2023 katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Grace Hamisi (mwenye ushungi wenye rangi nyeupe) akifanya mahojiano na Mtaalamu wa Fiziotherapia Mussa Chatila (Mwanaume) na Afisa habari wa hospitali hiyo Esha Mnyanga (mwenye ushungi wenye rangi nyeusi) kwenye kipengele cha afya ndani ya Kipindi cha Banjuka Weekend).

Jamii FM Radio kwa kushirikiana na Hospital ya Rufaa Kanda ya Kusini (SZRH) tumetoa elimu kwa jamii juu ya aina hii ya ulemavu ambao mtoto huzaliwa nao. Mtaalamu wa Fiziotherapia Mussa Chatila anafafanua juu ya hali hiyo pamoja na matibabu yake.

Afisa habari wa hospitali hiyo Esha Mnyanga anasema mtu asikae na tatizo bali afike hospitali ili aonane na wataalam wa afya kwani tatizo hilo linatibika kama akifuata taratibu na kumuwahisha mtoto kwa wakati.

Kwa wasiofahamu juu ya aina hii ya ulemavu ni kuwa Miguu kifundo au nyayo zilizopinda ni aina ya ulemavu unaotokana na matatizo ya mifupa . Ulemavu huu ni wa kuzaliwa nao na unaweza kumpata mtoto yoyote duniani.

Ulemavu huu husababisha maumivu makali wakati wa kutembea na pia unaweza kumsababishia mtoto kushindwa kwenda shule kutokana na unyanyapaa pamoja na kutengwa na wenzao katika jamii. Kwa mujibu taarifa  iliyotolewa mwaka 2019 na Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania – CCBRT takwimu zinaonyesha watoto 2500 mpaka 2800 wanazaliwa na hali hii kila mwaka hapa Tanzania.

Sikiliza mahojiano hayo

Kipindi: Ufahamu ulemavu aina ya Mguu kifundo au Unyayo uliopinda