Jamii FM

Wazazi watakiwa kutambua umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike

1 April 2024, 18:19 pm

Vera Assenga kutoka TGNP akiongoza mdahalo juu ya mila,tamaduni na changamoto zinazo mkwamisha Mwanamke kutoshiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi.(Picha na Musa Mtepa)

Imeelezwa kuwa chanzo kikubwa kinachosababisha watoto wa kike kutokufikia malengo  yao  ni wazazi kutotambua umuhimu wa elimu.

Na Musa Mtepa

Wazazi wametakiwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike  ili waweze kukabiliana na changamoto  za maisha pamoja na kuwa  majasiri kwenye  kupigania  nafasi za uongozi na maamuzi  katika  jamii .

Hayo yamesemwa 28/3/2024 na  mtendaji kata  wa kata ya Mkunwa  Aron Zephania Parsalaw  kwenye mdahalo  wa wazi  uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mkunwa ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambapo amesema kuwa  suala kubwa linalosababisha watoto wa kike kutofikia malengo  yao  ni wazazi kutotambua umuhimu  wa elimu .

Sauti ya Aron Zephania Parsalaw Mtendaji kata  wa kata ya Mkunwa

Akichangia mdahalo huo  Bw. Musa Liponda mkazi wa kijiji cha Mkunwa amesema kuwa ili mtoto wa kike avuke salama na kufikia umri wa kuwa kiongozi  lazima akwepe vikwazo vinavyosababisha mimba za utotoni vilivyoshamiri  katika jamii .

Sauti  ya 1 Musa Chiponda Mwananchi na mkazi wa kijiji cha Mkunwa

Aidha Bw. Liponda ameongeza kuwa mfumo na mitazamo ya malezi iliyopo kwenye jamii imekuwa ikichangia kwa asilimia kubwa kwa mtoto wa kike kutomaliza masomo yake.

Sauti  ya 2 Musa Chiponda mwananchi na mkazi wa kijiji cha Mkunwa

Kwa upande wake Vera  Assenga mwakilishi kutoka mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) amesema jamii ya wanamkunwa  kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha  anamlinda mtoto wa kike katika kufika malengo yake pamoja na ushiriki wa mwanamke katika nafasi za uongozi na maamuzi.

Sauti  ya Vera Assenga kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP

Naye  Coletha Chiponde  katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa  (KC) Mkunwa amesema  jukumu kubwa linalofanywa na kituo hicho ni kuelimisha  wazazi na watoto wa kike juu ya umuhimu wa elimu .

Sauti ya Coletha  Chiponde  katibu wa kituo cha taarifa na Maarifa (KC) Mkunwa