Jamii FM

TADIO kupambana na Magonjwa ya mlipuko

4 February 2021, 08:55 am

Shirika la Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO) limeanza kusambaza vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko vilivyotolewa na UNESCO Dar Es Salaam Office kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa vituo vya redio jamii chini ya mwamvuli wa TADIO.Vifaa hivi vyenye thamani zaidi ya TZS milioni 10 vinakusudiwa kufikia zaidi ya watendaji 300 wa redio na kusaidia waandishi wa habari kutoka vituo hivyo kujikinga na magonjwa ya milipuko katika shughuli zao za kila siku.

Wakati wa makabidhiano, mwenyekiti wa TADIO, Bwana Prosper Kwigize aliwataka mameneja wa redio wanachama wa TADIO kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinatumika vizuri na vinamfikia mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwandishi wa habari haswa waandishi wa habari wanawake.

Mameneja wa redio wanachama wa TADIO waliishukuru UNESCO na TADIO kwa msaada unaojali usalama wa wanahabari wa redio zao na waliahidi kuwa vifaa hivyo vitatumika kama ilivyokusudiwa.

UNESCO MISA Tanzania UNICEF UNICEF TANZANIA UNFPA UNFPA Tanzania Umoja wa Mataifa United Nations Tanzania Media Council of Tanzania IMS (International Media Support)
https://www.facebook.com/tadiotanzania/posts/1617854891732219