Jamii FM

Umeme upo wakutosha Mtwara na Lindi – TANESCO

9 March 2021, 11:57 am

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Mtwara limesema kwa sasa uzalishaji wa umeme Mtwara na Lindi umeongezeka na kupita kiwango cha matumizi ya mikoa hii ya Lindi na Mtwara na wanahakikisha kila mwananchi ananufaika na nishati hii ya umeme.

Mashine za kufua umeme wa gesi asilia zilizofungwa kwenye kituo cha uzalishaji Mtwara

Akitoa kauli hiyo mwishoni mwa juma, Meneja wa kituo cha uzalishaji umeme wa gesi asilia mkoa Mtwara Mhandisi Didasi Maleko amesema kulikuwa na mitambo ya kufua umeme yenye uwezo wa kuzalisha megawati 22.

Ameongeza kuwa kwa sasa serikali imeongeza mitambo na ili kuongeza mahitaji na kwasasa shirika linazalisha umeme megawati 30.4 kutoka megawati 22 za hapo awali.

Baadhi ya mitambo ya umeme iliyopo kwenye kituo cha uzalishaji umeme wa gesi asilia katika kituo cha Mtwara

Mahitaji ya umeme kwa mkoa wa Mtwara na Lindi kwa sasa ni megawati 18 kati ya megawati 30.4 zinazozalishwa na kituo na kufanya kubaki na nyongeza ya umeme unaozalishwa na shirika la umeme (TANESCO).