Jamii FM

Biteko awasha umeme wa REA Mtwara

16 November 2023, 13:13 pm

Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko akizungumza na wananchi wa kata ya Naliendele pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mtwara. Picha na Grace Hamisi

Na Grace Hamisi

Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Novemba 15,2023 amewasha umeme wa ujazilizi katika maeneo ya vijiji – miji awamu ya III mitaa ya Pachoto A, Pachoto B na Pwani kata ya Naliendele mkoani Mtwara.

Wananchi wa kata ya Naliendele wakimsikikiza Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko. Picha na Grace Hamisi

Sambamba na hilo amewapongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kusimamia vyema kazi ya kusambaza umeme, amewataka kutokucheka na wakandarasi hao ili kazi ya kupeleka mahitaji ya umeme kwa wananchi ifanyike kwa ufanisi.

Sauti ya Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Jones Olotu alimweleza Naibu Waziri Mkuu kuwa, Mkoa wa Mtwara umetengewa shilingi bilioni 170 kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini na kwamba katika vijiji 785 vya mkoa huo, Vijiji 401 bado havina umeme lakini wakandarasi kampuni ya Derm, Central na Namis wanaendelea kusambaza umeme kwenye Vijiji vilivyosalia.

Sauti ya Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Jones Olotu

Hata hivyo Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amezitaka kampuni zinazosimamia miradi ya umeme nchini Tanesco na Wakala wa Nishati vijijini (REA) kununua vifaa vya umeme vinavyozalishwa hapa nchini ili kukuza viwanda vya ndani, kuvipa thamani na kukuza ajira pamoja na uchumi wa Nchi.

Sauti ya Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko