Jamii FM
Jamii FM
5 June 2026, 10:49

Na Mwanahamisi Chikambu, Mwanaidi kopakopa
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mwamko mkubwa wa kutetea haki za binadamu, lakini bado kuna kundi linalosahaulika gizani ni wafanyakazi wa kazi za ndani. Katika mazingira ambayo kwa muda mrefu yamejaa unyanyasaji na ukimya, mabinti hawa wameanza kusimama imara kudai utu na haki zao ili kuleta mabadiliko chanya na usawa katika jamii yetu.
Katika kila kona ya nchi yetu, mabadiliko yanaanza kuchipua si kwa nguvu ya sheria pekee, bali kwa sauti za watu waliokataa kukaa kimya. Wengi wetu tunawaona asubuhi wakisafisha nyumba zetu. Wanatupikia, wanatunza watoto wetu, na kuhakikisha maisha yetu yanaenda sawa. Lakini, nyuma ya milango iliyofungwa na kuta za vyumba vyao, wasichana wengi wa kazi wanapitia mateso mazito yanayoumiza mioyo.