Jamii FM

Mwanafunzi: mkaa unanisaidia sana

16 April 2021, 07:54 am

Kauli ya “Kazi ziendelee inayotumika kama salam ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hasan imeendelea kuwafuta machozi Watanzania kwa kuwa kauli hiyo inazidi kuwapa nguvu na ari ya kuendelea kuchapa kazi na kulijenga Taifa letu.

Hamisi Mohamedi -Mwanafunzi wa Darasa la Sita shule ya msingi Nachenjele

Katika kuthibitisha hilo, Jamii fm radio imekutana na Mtoto Hamisi Mohamedi, mkazi wa kijiji cha Nachenjele, Mwanafunzi wa Darasa la Sita shule ya msingi Nachenjele iliyopo kwenye kata ya Mbawala Halmashauri ya wilaya ya Mtwara na kuzungumza nae baada ya mtoto huyo kutumia muda wake wa ziada kutengeneza Tanuru la mkaa ambapo ana matarajio ya kununua vifaa vya shule na pia kuwasaidia wazazi wake baada tu ya kuuza mkaa huo.

Hamisi amesema atauza mkaa huo kwa bei ya Sh 3000/= kwa Kiroba kimoja pale utakapokuwa tayari na amesema kuhusu wateja hakuna tatizo atawapata ndani ya kijiji hicho.

Jamii fm radio ilimuona mtoto huyo ikiwa kwenye harakati zake za kutafuta habari vijijini na kuzungumza nae. Hamisi amefurahia kuzungumza na Jamii fm Radio.