Jamii FM

Pembejeo za ruzuku zawafikia wakulima Mtwara

28 June 2023, 14:50 pm

Mchakato wa ugawaji wa pembejeo ya ruzuku kwa wakulima wa zao la korosho umeanza kuwafikia wakulima   katika maeneo mbalimbali  nchini.

Picha ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndugu Francies Alfred aliyeketi upande wa kushoto akizungumza na Mwandishi wa habari Mkongwe na mbobezi kwenye kilimo Ndugu Fakihi Musa aliyeketi upande wa kulia

Akizungumzia mchakato huo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndugu Francies Alfred amesema kuwa kwa miaka miwili iliyopita ugawaji wa pembejeo ulikuwa unasimamiwa na vyama vikuu vya ushirika kugawa pembejeo hizo hali iliyopelekea changamoto ya upotevu  hivyo kulazimika kubadilisha mfumo huo.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndugu Francies Alfred

Sambamba na hilo  Bw Francis  amesema kuwa kwa wale wote ambao walishindwa kujisajili  katika awamu ya kwanza  ya usajili watasajiliwa  awamu ya pili na matarajio ya upatikanaji wa pembejeo  ni kwa awamu ya pili pia.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndugu Francies Alfred

Aidha mkurugenzi mkuu wa bodi ya korosho ametolea ufafanuzi juu ya utolewaji wa pembejeo ya ruzuku inayotolewa na serikali huku akiwataka wakulima kutotegemea  pembejeo ya ruzuku pekee katika kuhudumia mashamba yao.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndugu Francies Alfred