Jamii FM

Brela yawapiga msasa maafisa biashara mikoa 10

12 May 2023, 18:00 pm

Na Msafiri Kipila

Wakala wa leseni za biashara Brela wameendesha mafunzo ya siku 3 kwa maafisa biashara wa mikoa 10 ya kanda ya kusini na nyanda za juu kusini, yamefanyika hapa mkoani Mtwara lengo ikiwa ni kutatua changamoto zinazo wakabili.Wakizungumza katika kuhitimisha mafunzo hayo Afisa Biashara Mohamed Kiguga amesema mafunzo ayo yatawapa faida kubwa ya kubadilika katika utendaji wao wa kazi

Maafisa biashara 100 kutoka mikoa 10 ya kanda ya kusini na nyanda za juu kusini wakiwa kwenye mafunzo mkoani Mtwara (picha na Msafiri Kipila)

Sauti ya Mohamed Kiguga Afisa biashara Wilaya ya Malinyi Morogoro

Sada Salumu Lukala afisa biashara kutoka Nyasa kutoka Mkoa wa Ruvuma amesema mafunzo yatawasaidia kuwapatia wananchi elimu ili kukuza uchumi wan chi na kuwasaidia kwenye kuwajengea uwezo wananchi na kutatua changamoto zao ikiwemo ya upatikanaji wa leseni.

Sauti ya Sada Salumu Lukala afisa biashara wilaya ya Nyasa Ruvuma.

Kaimu mkuu kutoka BRELA TAWI GODI FREY KILUMILE Amesema mafunzo hayo yatawezesha maafisa biashara katika kuwajengea uwezo na uwelewa kwaajili ya kuimalisha na kuboresha utendaji kazi kwa maafisa biashara kwa kua wapo karibu na wafanyabiashara.

Sauti ya Tawi Godfrey Kilumile

Katika kufunga mafunzo hayo Mkuu Wa Mkoa Mtwara Kanali Ahmed Abasi amehitimisha mafunzo hayo kwa kuwapongeza waandaji wa mafunzo haya na wale wote walioshiriki mafunzo hayo.

Lakini pia Amewataka maafisa biashara kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo kuepuka kufanya kazi kwa mazoea .

Sauti Mhe Kanal Ahmed Abasi- mkuu wa mkoa wa Mtwara.