Jamii FM

Waziri Mkuu asisitiza kuainisha ubadhirifu kwenye miradi itakayopitiwa na mwenge

1 April 2023, 23:18 pm

Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kasim Majaliwa akikabidhi mwenge wa Uhuru. Picha na Mussa Mtepa

Na Mwandishi wetu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wakimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa kukagua miradi yote kwa umakini na kuishauri Serikali hatua za kuchukua kwa kila mradi.

Muende mkakague miradi ya maendeleo na kuainisha ubadhirifu na msisite kutoa mapendekezo nini kifanyike katika miradi mtakayotembelea

Akizindua mbio za mwenge wa uhuru kitaifa leo April 1, 2023 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara Mh Majaliwa, amesema waende kukagua miradi ya maendeleo na kuainisha ubadhirifu na wasisite kutoa mapendekezo nini kifanyike katika miradi watakayotembelea.

Kaulimbiu ya mwenge wa uhuru kwa mwaka huu unasema “Tunza mazingira, Okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa taifa”.

Kilele za kuzima mwenge wa Uhuru kinatarajiwa kufanyika Mkoani Manyara October 14, 2023

Ujumbe huo umelenga katika kuhifadhi mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji, kupinga rushwa, kupinga ukatili wa wanawake, watoto na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2023 ni Abdallah Shaib Kaim kutoka mkoa wa Kaskazini Pemba, akisaidiwa na Martin Michael Mkanga kutoka Mtwara, Atupokile Elia Mhalila kutoka jijini Dodoma, Juma Silima Sheha kutoka Mkoa Kaskazini Unguja, Zainabu Hemedi Mbetu kutoka Mkoa Kaskazini Unguja na Emmanuel Jackson Hondi wa Mkoani Manyara.

Kilele za kuzima mwenge wa Uhuru kinatarajiwa kufanyika Mkoani Manyara October 14, 2023 mara baada ya kukimbizwa katika mikoa yote 30 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania