Jamii FM

TANESCO Mtwara watoa elimu kwa wajasiliamali

7 February 2021, 11:06 am

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Mtwara, wametoa elimu ya matumizi sahihi ya umeme kwa wajasiliamali mkoani hapa baada ya kuwatembelea kwenye sehemu zao za Biashara Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Mhandisi Aurea Bigirwamungu ambae ni Afisa mkuu wa utafiti TANESCO makao makuu akizungumza na wajasiliamali katika eneo la Mnarani Manispaa ya Mtwara Mikindani kwenye mashine za Kusaga nafaka

Akitoa elimu hiyo mhandisi Aurea Bigirwamungu ambae ni afisa mkuu wa utafiti TANESCO Makao makuu amesema, wameamua kutoa elimu hiyo kwa wajasiliamali wa mkoa wa Mtwara  ili waweze kutumia ipasavyo nishati ya umeme ili kuboresha biashara zao na kwendana na kasi ya uchumi wa kati.
Pia wametumia fursa hiyo kusikiliza changamoto mbalimbali za wajasiliamali zinazowakabili na kuwahaidi kuzifanyia kazi ili kuleta tija ya upatikanaji  wa nishati ya umeme ya uhakika kwa mkoa wa Mtwara na Lindi.