Sampuli ya madawa ya kulevya
Jamii FM

Mama mjamzito akitumia dawa za kulevya zinamuathiri mtoto kuanzia tumboni

31 January 2023, 12:06 pm

Mfamasia wa kitengo cha kinga ya tiba Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya  Upendo Chenya. Picha na Gregory Millanzi.

Mama mjamzito anayetumia madawa ya kulevya ana kiwango kikubwa cha kumuathiri mtoto akiwa tumboni, na wengi wao wanapoteza maisha wakati wa kujifungua.

Na Gregory Millanzi

Mama mjamzito akiwa anatumia madawa ya kulevya zinamuathili mama kwenye mfumo wake wa  uzazi na kupelekea mtoto kuathirika moja kwa moja kama ambavyo mama anaathirika kwa dawa hizo, na kupelekea mtoto kuwa na uraibu na wakati mwimgine husababisha vifo kwa mama mjamzito wakati wa kujifungua.

Akizungumza na Jamii FM Radio  Mfamasia wa kitengo cha kinga ya tiba Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya  Upendo Chenya  amesema, madawa ya kulevya kwa mama mjamzito ni jambo baya  sana kwa  afya ya mama na mtoto mtarajiwa, kwani mama mjamzito wakati anatumia madawa ya kulevya atahri za dawa zinaenda kumuathiri mtoto moja kwa moja.

Ameongeza kuwa, mama mjamzito anayetumia madawa kuna wakati anakuwa na uhaba wa kupata madawa(alosto), ile hali huwa inamtesa sana mama na ndivyo hivyo hivyo pia mtoto akiwa tumboni anateseka pia na alosto ya mama.

Upendo amesema, madawa ya kulevya hupenya kwenye mfuko wa uzazi wa kumtunza mtoto (Placenta), kwa sasababu dawa hizo zinapenya  kwahiyo zinaathari ya moja kwa moja kwa mtoto, na atahari zake ni zile anazozipata mama na mtoto anazipata moja kwa moja,na hali hii upepekea vifo vya mama wengi wenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Mfamasia wa Kitengo cha Kinga na tiba Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Upendo Chenya amesema, kwa sasa wanawanusuru watoto wanaozaliwa  wakiwa na uraibu wanawapatia dawa ili aweze kuachana na uraibu na baada ya muda ndio wanamrudisha kwa mama yake kwa ajili ya kuanza kunyonya maziwa ya mama ambayo nayo yanadawa.

Kwa upande wake  Kamishna msaidizi  kinga na huduma za Jamii  tiba Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Moza Makumbuli amesema kuwa, wanawake wengi wanapokuwa wanatumia madawa ya kulevya hupoteza mzunguko wao wa mwezi,na hali hiyo wakati mwingine hupelekea kupata mimba bila wao kujijua.

Makumbuli ametoa wito kwa wanachi wote kuacha au kutotumia kabisa dawa za kulevya kwasababu sio nzuri kiafya na zinapoteza utu wa mtu, amewasihi wale ambao wanatumia na wanataka kuacha wanatakiwa kwenda kwenye vituo vya uangalizi na kuacha kutumia kabisa.