Jamii FM

RC Mtwara akabidhi vifaa vya TEHAMA kwa walimu

23 April 2024, 16:58 pm

RC: Kanali Patrick Sawala akikabidhi tv ikiwa moja ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa maafisa Elimu kutoka vituo 10 vya Walimu Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Vifaa hivi vitasaidia walimu kupakua na kujiongezea maarifa kupitia mtandao ambayo yatasaidia katika kuboresha hali ya ufaulu katika shule zetu

Na Musa Mtepa

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala  Leo tarehe 23/4/ 2024 amekabidhi vifaa vya TEHAMA kwa vituo 10 vya walimu (TRC) kupitia Mradi wa Boost vyenye thamani ya shilingi Milioni 343 za kitanzania.

Akikabidhi   kwa wawakilishi wa Vituo 10  mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Partick Sawala amewataka kuvitunza  vifaa hivyo  na kuvitumia kwa malengo yaliyopangwa  ili kuleta matokeo  tarajiwa kupitia  utendaji kazi katika maeneo yao  ikiwemo katika kusaidia na  kuwezesha Walimu  kujifunza mbinu balimbli za ufundishaji na ujifunzaji kupitia  mpango endelevu wa  mafunzo  ya Walimu kazini (MEWAKA).

Sauti ya 1 Kanali Patrick Sawala Mkuu wa  mkoa wa Mtwara

Pia  Kanali Patrick Sawala  amewaelekeza wakuu wa Wilaya  kuwa karibu na kwenda kufuatilia  kwenye maeneo yao kuona  vifaa hivyo vinatumika kama ilivyopangwa  au vinginevyo  na pia  akizitaka Halmashauri zote kuhakikisha zinaajiri walinzi watakao linda vituo vya Walimu (TRC) ambako vifaa hivyo vinaenda kutumika.

Sauti ya 2 Kanali Patrick Sawala Mkuu wa  mkoa wa Mtwara
RC: Patrick Sawala akipitia taarifa ya vifaa vilivyo kabidhiwa kwa vituo 10 vya walimu mkoani Mtwara.(Picha na Musa Mtepa)

Aidha kwa upande wake Mratibu wa mradi wa Boost mkoa wa Mtwara Mwalimu Dadi Ngahalo amesema vifaa hivyo vinaenda kutumika kwenye vituo  vya Walimu 10 kwa ajili ya kuboresha mafunzo ya Walimu kazini kupitia mpango  Endelevu wa mafunzo ya walimu kazini (MEWAKA)

Sauti ya Mwalimu Dadi Nagahalo Mratibu wa Mradi wa Boost mkoa wa Mtwara
Maafisa Elimu kutoka vituo 10 vya Walimu wakisikiliza hotuba ya mkuu wa mkoa katika hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA kwa vituo hivyo(Picha na Musa Mtepa)

Naye Shakila Omari Mkwazo  na Mohamedi Kazumari  maafisa Elimu kutoka kata ya Mitengo na Kilomba wamesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia Walimu katika kuongeza ufaulu kwa  Shule mbalimbali kwa kuwa Walimu watakuwa wakipata  na kuongeza maarifa mapya kupitia vifaa hivyo.

Sauti ya Shakila Omari Mkwazo  na Mohamedi Kazumari maafisa Elimu kutoka kata ya Mitengo na Kilomba mkoani Mtwara.