Jamii FM

Madiwani Mtwara fanyeni Kazi za maendeleo

5 February 2021, 08:00 am

Waheshimiwa madiwani wa manispaa ya mtwara mikindani mkoani Mtwara wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kujipatia maendeleo. Hayo yamesemwa na Afisa tawala Idara ya serikali za Mitaa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Mtwara Bi Edith Shayo, katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 04.02.2021 katika ukumbi wa shule ya sekondari Call and Vision Mtwara.

Afisa tawala Idara ya serikali za Mitaa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Mtwara Bi Edith Shayo