Jamii FM

Mila, desturi kikwazo wanawake kuwa viongozi

21 June 2023, 13:40 pm

Mila na tamaduni zinachukua nafasi kubwa katika kuenzi nafasi za wazee katika jamii zetu, wandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kupunguza baadhi ya mila zenye kuharibu jamii hasa wanawake.

Na Musa Mtepa

Wandishi wa habari mkoani Mtwara wameelezea changamoto zinazowasababishia  wanawake  wengi kutojihusisha katika nyadhifa mbalimbali za uongozi huku  sababu ikielezwa kuwa  utamaduni na imani ya dini ndio kikwazo kikubwa.

Katibu msaidizi wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Mtwara Gregory Millanzi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Wakizungumza baada ya mafunzo ya siku mbili Juni 19-20, 2023 yaliyohusu kumwezesha mwanamke kuingia na kujihusisha kwenye uongozi katika jamii chini ya shirika lisilo la kiserikali la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wamesema kuwa mila, desturi na imani ndio kikwazo kikubwa kwa wanawake wa mkoa wa Mtwara kutojihusisha na masuala ya uongozi.

Sauti za wandishi wa habari wa mkoa Mtwara.
Deogratusa Temba wa TGNP akizungumza na wandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Deogratus Temba amesema kutokana na majadiliano wamebaini kuwa baadhi ya mila na desturi zinazofanyika katika jamii hupelekea mwanamke kutoshiriki katika nyazifa za uongozi na wakati mwingine jamii hujenga taswira ya mwanamke kumweka kuwa dhaifu katika jamii.

Sauti ya Deogratusa Temba wa TGNP