Jamii FM

Waziri Jafo ataka tathmini ya Mazingira ifanyike

26 July 2023, 08:06 am

Mamlaka ya bandari imepewa miezi mitatu ili kufanya ukaguzi wa mazingira (Environmental Audit) ili kuhakikisha Kuna ubora wa biashara ya makaa ya mawe

Na Grace Hamisi

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mh. Selemani Jafo, amelidhishwa na uwepo wa mitambo ambayo hutoa maji kwa lengo la kupunguza vumbi kwenye makaa ya mawe bandarini na uwepo wa uzio unaozuia vumbi katika eneo la kuhifadhi makaa ya mawe.Waziri Jafo ameyasema hayo julai 24, 2023 alipotembelea bandari ya kuu ya mkoa wa Mtwara

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Selemani Jafo (katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbasi (kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh. Hanafi Msabaha (Kulia)

kwenye ziara yake ya kikazi ya Waziri Jafo ametoa miezi mitatu kwa mamlaka ya bandari kufanya ukaguzi wa mazingira (Environmental Audit) kwani hii itasaidia kuwepo kwa ubora wa biashara hiyo ya makaa ya mawe kwa nchi nyingine

Sauti ya waziri Jafo

“Nataka ndani ya miezi mitatu muwe mshamaliza environmental audit kwani tunachohitaji makaa ya mawe yanayotoka Tanzania kwenda nchi yoyote yaonekane makaa hayo yametoka kwenye nchi ambayo mazingira yake yalilindwa kwa sababu kuna ya bidhaa nyingine zikionekana nchi flani zinasafirishwa bidhaa bila ya kujali mazingira inawezekana katika soko la dunia wakaiblacklist hiyo biashara” anasema Jafo

Kwa mara ya kwanza alitoa maagizo hayo Decemba 2021 wakati wa ziara yake mkoani Mtwara baada ya malalamiko ya wananchi kuwepo wa changamoto ya vumbi na umwagaji wa makaa ya mawe kwani kulikuwa na mazingira hatarishi