Jamii FM

Mvua zasababisha kifo

14 January 2021, 04:46 am

Kutokana na mvua kubwa zilizonyesha siku mbili mfululizo katika manispaa ya Mtwara mikindani,imesababisha kifo cha mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ally Machulila (65) dereva pikipiki aliyesombwa na maji alikuwa anakatiza kwenye maji na kuzidiwa na kusababisha umauti, pia baadhi ya nyumba zimeathirika kwa kuzingilwa na maji.

Akitoa taarifa ya pole kwa maafa hayo mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ametaja maeneo yaliyoathirika zaidi na mvua kwa manispaa ya Mtwara mikindani ni Naliendele, Ligula, kiangu, magomeni matopeni, likonde, Chipuputa, Mangamba na maeneo hayo yote yamezungukwa na maji kwenye nyumba zao.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ametoa taarifa hiyo kwenye kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa tawi la benki kuu Mtwara na kuwaomba Wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) na wakala wa barabara Tanzania (TANROAD) kuakikisha wanakarabati barabara zilizoharibiwa na mvua ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kama ilivyokuwa hapo awali.