Jamii FM

Mtwara: Watu 15 watuhumiwa kwa Viuatilifu feki

31 July 2021, 15:18 pm

Na Musa Mtepa.

Jumla ya Tani 84.3 za pembejeo Feki (Viuatilifu) zenye thamani ya Zaidi ya milioni 100 zimekamatwa katika oparesheni maalumu wakati zikipelekwa Kwa wakulima wa zao la korosho mkoani Mtwara.

Mkuu wa Mkoa Mtwara Brigedia Jeneral Marco Elisha Gaguti akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake

Akizungumza Na waandishi WA Habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa Mtwara Brigedia Jeneral Marco Elisha Gaguti amesema kuwa pembejeo hizo zilizokwisha muda wake zimekamatwa katika wilaya Tandahimba, Manispaa ya Mtwara mikindani na nyinginezo katika wilaya ya Newala, Masasi na Nanyumbu.

Aidha Mkuu wa mkoa amewataka wakulima kuwa makini wakati wa ununuzi wa pembejeo kwani Wafanya Biashara wengi wapo Kwa ajiri ya maslahi yao binafsi na sio Kwa ajili ya wakulima.

Pia Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kutoa taarifa Kwa vyombo vya usalama pindi wanapobaini uwepo wa pembejeo feki Ili kuthibiti na kuboresha uzalishaji wa zao la korosho Kwa mkoa wa Mtwara na Tanzania Kwa ujumla.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mark Njera akionyesha pembejeo zilizokwisha muda wake wa matumizi, ambazo zilikuwa tayari kwa ajili ya kwenda kwa wakulima kwa ajili ya matumizi (PICHA NA GREGORY MILLANZI, Mtwara)

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi Mark Njera amesema kuwa Kwa kushirikiana vyombo vya usalama mkoa wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 15 baada ya operesheni ya siku mbili kati ya tarehe 28/29 mwezi July na kubaini kuwa walitumia nyaraka za kughushi kuhalarisha pembejeo hizo ikiwemo kutumia barua feki kutoka Kwa mamlaka inayosimamia na kutoa ruhusa juu uzaji na usambaji wake.

Aidha Kamanda Njera amesema kuwa watuhumiwa wanaendelea na mahojiano na upelelezi utakapo kamilika watapelekwa mahakamani na sheria ichukue mkondo wake.

Naye katibu wa ununuzi wa pembejeo wa zao la korosho nchini ambae pia ni Meneja wa TANECU amesema kuwa wakulima hawana budi kuwa makini Kwa kujiridhisha muda Na mwaka pembejeo hizo zilipo zalishwa Ili kuondoa uzalishaji dhaifu wa zao la korosho utakaosababishwa na Pembejeo zilizopitwa na wakati.