Jamii FM

Kipindi: Wenye ulemavu wanavyoweza kuibadilisha jamii kivitendo na mtazamo

11 April 2023, 12:17 pm

Mwalimu Getrude Jonas Bukengwa akizungumza na Musa Mtepa. Picha na Amua Rushita

Na Musa Mtepa

Mifumo ya usaidizi ni muhimu ili watu wenye ulemavu waweze kuishi maisha yenye utu, waweze kujitegemea na wawe huru zaidi, haya ni maneno yaliyosemwa Machi 13 2023 kwenye mkutano wa  ‘’Mtazamo wa Kimataifa wa Habari za kiutu’’ huko Geneva, Uswisi  na Mtaalamu Huru wa kutoka Umoja wa Mataifa  Bw Gerard Quinn  kuhusu watu wenye  ulemavu.

Ambapo Katika ripoti   iliyowasilishwa kwenye  Baraza la Haki za Kibinadamu kwa mujibu wa azimio la 44/10 la Baraza, amesema kuwa  haki za watu wenye ulemavu  lazima zizingatiwe ikiwepo kupata  Elimu, kuishi, Afya, Malazi, chakula, Faragha na huduma nyinginezo ambazo watu  wenye utimilifu wa viungo wanapata.

Leo nikikukaribishe kwenye kipindi hiki ambapo  tunaangazia ni jinsi gani Watu wenye ulemavu  wakipewa mahitaji  sawa na wenye viungo timilivu wanavyoweza kuibadilisha jamii kivitendo na mtazamo.

Mwalimu Getrude akibadirishana mawazo na ndugu Said. Picha na Amua Rushita

Mwandaaji  na msimuliaji wa kipindi hiki ni mimi Musa Mtepa wa jamii fm Radio

Kupitia kipindi hiki tunazungumza na Getrude Jonas Bukengwa  Mlemavu wa miguu anaetembea kwa msaada kiegemeo(Magongo)  akituelezea  safari yake ya Masomo hadi kuwa Mwalimu wa shule ya msingi  jamii ilivyo mchukulia lakini pia Ndoto zake kwa siku za usoni.

Mazungumzo ya Musa Mtepa na Mwalimu Getrude Jonas Bukengwa ambaye ni Mlemavu wa miguu anaetembea kwa msaada kiegemeo(Magongo)

Naaam tumepata kusikia,kujifunza na kuelemika kupitia Dada Getrude Jonas Mwalimu wa shule ya Msingi Shangani iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani juu ya maisha aliyopitia hadi kuwa Mwalimu na matamanio aliyokuwa nayo kwa siku za usoni huku kubwa akiwataka wadau wa Elimu kam vile taasisi Binafsi na Serikali kuhakikisha wanajenga miundombinu  rafiki kwa watu wenye ulemavu  na kuendelea kutoa Elimu kwa wazazi kuona umuhimu wa kuwasomesha watoto wenye ulemavu .

Aidha  Mwalimu Getrude amesema kuwa jamii imekuwa na kasumba la kuwatenga watu wenye ulemavu hususani katika mahitaji ya msingi kama vile Elimu  hivyo jamii iachane na kasumba hiyo na kuwapatia elimu kwa msaada  wa maisha ya baadae.

Hadi kufikia hapo sina la ziada muandaaji na msimulizi wa kipindi hiki ni mimi Musa Mtepa wa jamii fm Radio Mtwara.