Jamii FM

Wafanyabiashara wa Soko la Chuno, wafanya vurugu

5 May 2021, 16:31 pm

Na Gregory Millanzi

Wafanyabiashara katika soko la Chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wameilalamikia serikali kuruhusu wafanyabiashara wa soko la sabasaba kufanya Biashara katika soko hilo ambalo mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa aliamuru biashara zote za jumla lihamishwe chuno.

Wafanyabiashara katika Soko la chuno Mkoani Mtwara

Pia wafanyabiashara wa Soko la chuno manispaa ya Mtwara Mikindani wamewashinikiza wafanyabiashara wa Soko la sabasaba ambae anamiliki kizimba ndani ya Soko la Chuno aondoke sokoni hapo.

Baadhi ya wafanyabiashara wameiomba wameiomba serikali kuingilia Kati suala na kudai hali ya kibiashara katika soko la chuno hairidhishi.

Wafanyabiashara wa Soko la chuno wakijadiliana wakati wa vurugu

Soko la Chuno lenye ukubwa wa gorofa moja , wapo wafanyabiashara waliopata vizimba juu na chini lakini baadhi havitumiki na wahusika.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha biashara manispaa ya Mtwara Mikindani Frank Ndebeka amesema hili tatizo linaendelea kufanyiwa kazi na wanaendelea kuhakikisha wafanyabiashara wote wanafanya Kazi kwenye Soko moja ila kuna kesi mahakamani iliyofunguliwa na baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba.

Machi 11 Mwaka huu mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa alifanya mkutano wa hadhara na wafanyabiashara wa Soko la sabasaba na kuwaamuru kuhamia Soko la Chuno ndani ya siku saba.