Jamii FM

Makala: Hali ya upatikanaji wa chakula shuleni

23 June 2024, 10:00 am

.Mwanafunzi wa darasa la awali wa Shule ya Montessori akiosha chombo chake baada ya kumaliza kupata chakula cha Mchana. Picha na Gregory Millanzi

Imeandaliwa na Gregory Millanzi pamoja na Mwanahamisi Chikambu

Chakula ni kitu chochote kinacholiwa ambacho huupa mwili nguvu na joto. Ni lishe inayompa mtumiaji virutubisho vyote vinavyohitajika na mwili kwa kiasi kinachozingatia kanuni za afya.

Serikali ya Tanzania imeanzisha Huduma ya Chakula Shuleni kama njia ya kuboresha elimu na umakini wa wanafunzi wakiwa shuleni, na hivyo kuongeza ufaulu wao. Hii inalenga kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata lishe bora wanapokuwa shuleni.

Hata hivyo, kuna uelewa mdogo miongoni mwa jamii kuhusu umuhimu wa utoaji wa chakula shuleni, hasa katika jamii nyingi za Tanzania. Wazazi wengi wanahisi kuwa kuchangia chakula shuleni ni upotevu wa fedha au ni matumizi mabaya, bila kuelewa kwamba chakula hiki kinachangwa kwa kuzingatia mahitaji ya lishe ya watoto wao. Aidha, baadhi ya wazazi wanadhani ni rahisi zaidi kwa mtoto kurudi nyumbani kwa ajili ya chakula, bila kuzingatia umbali au mazingira ya shule.

Wanafunzi wa darasa la kwanza na awali shule ya msingi Nanguruwe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, wakiwa kwenye mapumziko. Picha na Gregory Millanzi

Katika makala hii, tunazungumzia hali ya upatikanaji wa chakula shuleni, hasa kwa wanafunzi wa Darasa la Awali na Darasa la Kwanza. Muandaaji wa makala haya ni Gregory Millanzi akishirikiana na Mwanahamisi Chikambu kutoka Jamii FM Radio.

Ikumbukwe kwamba:

– Chakula ni muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya watoto wadogo shuleni.

– Utoaji wa chakula shuleni unachangia kuboresha masomo na umakini wa wanafunzi.

– Elimu kwa jamii ni muhimu ili kuelewa faida za huduma ya chakula shuleni.

– Wazazi wanahitaji kushirikiana na shule kuhakikisha watoto wao wanapata lishe bora wanapokuwa shuleni.

Bonyeza hapa kusikiliza makala haya