Jamii FM

Uzinduzi msimu utalii wa nyanguni Msimbati

9 August 2023, 17:56 pm

Wadau wa utalii wakiwa katika fukwe za Msimbati mkoani Mtwara

Na Grace Hamisi

Wananchi wa kata ya Msimbati mkoani Mtwara wametakiwa kujipanga na kupokea mabadiliko juu ya wageni wanaotembelea na kujifunza vivutio mbalimbali vilivyopo katika maeneo hayo.

Wito huo umetolewa August 5, 2023 na Bi Esha Chilonda afisa mtendaji wa kata ya Msimbati wakati wa uzinduzi wa msimu wa utalii wa nyangumi ambapo amesema kuwa Msimbati ni eneo lililo barikiwa na uwepo wa vivutio mbalimbali ikiwemo Milima ya Mchanga, fukwe za kuvutia, visima vya gesi na makundi ya wanayama bahari aina ya nyangumi hivyo wananchi wanatakiwa kujipanga katika miundombinu ya malazi, chakula, usafiri pamoja na ukarimu ili kuendana na fursa hizo.

Mkuu wa mkoa wa mtwara katika uzinduzi wa utalii wa Nyangumi katika eneo la Msimbati

Akizindua zoezi hilo mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Ahmedi Abbas amesema kuwa wawekezaji mbalimbali waje kuwekeza ndani ya mkoa wa Mtwara kwani ni sehemu salama, tulivu na inakila sababu ya kuweka mazingira ya uwekezaji kuwa rafiki.

“Wawekezaji waje kujenga hoteli, waje kufanya uwekezaji safari za boti za kubeba wageni kuwapeleka maeneo mbali mbali ya vivutio vilivyopo mkoani Mtwara” amesema Kanali Abbas

Pia Mkuu wa mkoa amewataka Wananchi wa Mtwara kutumia fursa ya uwepo wa makundi ya Nyangumi katika kipindi hiki cha ujio wao kwani ni urithi ambao unakila sababu ya kuutangaza na kuendeleza kwa faida ya Mtwara na nchi kwa ujumla.Kwa upande wake afisa Muhifadhi Mfawidhi wa Hifadhi ya Bahari ya huba ya Mnazibay na maingilio ya Mto Ruvuma

Redfrey Ngowo amesema kuwa eneo la hifadhi linaukubwa wa kilomita za mraba 650 ambapo kati ya hizo kilomita 430 ni eneo la maji linalopatikana Wanyama aina ya Nyangumi ambao wamekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutembelea eneo hilo huku zaidi ya watalii (Wageni) 560 kwa mwaka 2022 na 630 kwa mwaka 2023 wakitembelea kujionea wanyama hao.

Aidha Redfrey Ngowo amesema kuwa nyangumi ni mnyama bahari mwenye akili na mwenye kutambua mazingira rafiki kwa kuishi hivyo kutokana na kuongezeka kwa hali baridi ya Bahari ya kusini Mwa afrika kila mwaka ifikapo mwezi july hadi November wamekuwa wakipatiana katika eneo la Msimbati.