Jamii FM

Waomba Shule ifunguliwe

7 February 2021, 12:18 pm

Wananchi wa kijiji cha Tangazo halmashauri ya wilaya ya Mtwara mkoani hapa wameiomba serikali wafungue shule ya sekondari Tangazo kwa kuwa watoto wao wanatembea umbali wa zaidi ya km 20 kwenda na kurudi shule ya sekondari Mahurunga hali inayopelekea baadhi yao kukatisha masomo. Akiongea na Jamii fm radio, Diwani wa kata hiyo Mh Mohammedi Muwanya ameishukuru serikali kwa kuwajengea shule hiyo ambapo itasaidia kuinua kiwango cha elimu maana kutokana na umbali wanaotembea wanafunzi wa kijiji hicho wanakutana na vikwazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto wa kike kurubuniwa na wanaweza kushika ujauzito. Nae Afisa elimu sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Mtwara Mwalimu Fadhili Mvungi amesema anajiandaa kwenda Dodoma kufuatilia usajili wa muda na Shule hiyo itafunguliwa ndani ya mwezi huu wa pili huku akiwataka wanafunzi hao kuyatunza majengo yao pindi watakapoanza masomo.

shule ya sekondari Tangazo