Jamii FM

Wagonjwa 4500 kunufaika na kliniki ya macho Mtwara

26 April 2024, 20:35 pm

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Shadida Ndile akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye kliniki ya macho kwenye viwanja vya shule ya sekondari Mitengo(Picha na Musa Mtepa)

Chanzo kikubwa ni umri wengi waliokutwa na tatizo la macho ni wale wenye umri kati ya  miaka 60/ 70 na wengine walikuwa na hatari kidogo na hawakutibiwa mapema hivyo macho yao yamaeingia ukungu na hawakuweza kutolewa na leo wametolewa na kesho ikifika watakuwa wanaona  kabisa

Na Musa Mtepa

Zaidi ya wagonjwa 4500 wa macho wanatarajia kunufaika na kambi ya siku tatu ya kliniki ya macho  iliyozinduliwa leo Tarehe 26/4/2024 katika viwanja vya shule ya sekondari Mitengo Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Akizindua kambi hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani  Mheshimiwa Shadida Ndile amesema kuwa tatizo la macho ndani ya mji wa Mtwara ni kubwa hivyo uwepo wa kambi hiyo itawasaidia wananchi wengi wenye uhitaji wa huduma sndani ya mji wa Mtwara na mkoa kwa ujumla.

Sauti ya 1 Shadida NdileMeya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani

Pia Mstahiki Meya amewataka wanamtwara kuchangamkia fursa hiyo inayotolewa bure na kituo cha KSI kwa kushirikiana na mtandao wa Simu wa tigo Tanzania  ili kuepuka gharama kubwa zinazotolewa  kwenye hospitali na vituo vya afya nchini.

Sauti ya 2 Shadida Ndile Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa tigo kanda ya Pwani  Bw Aidani Komba amesema kuwa kwa kushirikiana na kituo cha KSI wamewezesha upatikanaji wa huduma za matibabu ya macho kwa wakazi wa Mtwara na maeneo Jirani ambao wangepata ugumu katika kupata huduma hizo.

Sauti ya Aidani Komba mkurugenzi mtendaji wa mtandao was imu wa tigo Tanzania kanda ya pwani

Mkurugenzi wa mtandao wa simu za mkononi wa tigo kanda ya Pwani Aidani Komba akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye kliniki ya macho kwenye viwanja vya shule ya sekondari Mitengo(Picha na Musa Mtepa)

Naye kaimu mganga mkuu ambae pia ni mratibu wa huduma za tiba Manispaa ya Mtwara mikindani Daktari Perensian  Rwezaula amesema hali ya ugonjwa wa macho kwa  Mtwara mikindani bado kuna changamoto ya  wagonjwa wengi na wengiwao wakiwa wazee watu wazima na wa kuzaliwa nao.

Sauti ya Daktari Perensian Rwezaula kaimu mganga mkuu na mratibu wa tiba Manispaa ya Mtwara Mikindani

 Bi Elizabeth Mpili mkazi wa Mtaa wa Mangoela Manispaa ya Mtwara Mikindani amekishukuru kituo cha KSI na Mtandao was imu za mkononi wa tigo kwa kupata huduma ya macho bure huku akiwaomba Wananchi wa mtwara Kujitokeza kwa uwingi  kupata huduma hiyo.

Sauti ya Bi Elizabeth Mpili Mwananchi mnufaika wa huduma za macho mkazi wa mtaa wa Mangoela Mtwara mjini

Kwa mujibu wa  mratibu wa kambi hiyo Hassani Omari Dinya kutoka Bilali Muslim amesema huduma hiyo itatolewa kwa muda wa siku tatu kwa kuanzia tarehe 26/4/2024 hadi 28/4/2024 katika viwanja vya shule ya sekondari Mitengo huku malengo yakiwa kuhudumia wagonjwa 1000 hadi 1500m kwa siku.

Sauti ya Hassani Omari Dinya mratibu wa kambi ya siku tatu kutoka Bialali Muslim
Wananchi wa Mtwara waliojitokeza kwenye kliniki ya macho kwenye viwanja vya shule ya sekondari Mitengo(Picha na Musa Mtepa)