Jamii FM

Kampeni ya kugawa Taulo za kike kwa Wanafunzi Mtwara yaanza

1 December 2020, 11:59 am

Baadhi ya wanafunzi wa shule za Sekondari Mkoani Mtwara

Moja kati ya changamoto kubwa inayowakumba  watoto wakike walioko shuleni  hadi kupelekea kujiingiza katika mahusiano wakiwa na umri mdogo ni suala la upatikanaji wa taulo za kike, hii imekuwa changamoto kubwa kwa mabinti wengi. Kwa kulitambua hilo  Mwanaidi Simba  Kutoka mkoani  Mtwara ameanzisha kampeni ya “TUSIMAME NAO”  kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wakike kwa kuwapatia taulo za kike shuleni ili ziweze kuwasaidia pindi wanapoingia kwenye siku zao ,Ambapo siku ya kesho tarehe 2/12/2020 ataanza zoezi hilo katika shule ya msingi Lilungu iliyopo manispaa ya Mtwara Mikindani.

Mwanaidi Simba akiongea na Jamii Fm