Jamii FM

MAKALA – Uanzishwaji ngo’s na changamoto wanazokutana nazo

1 May 2023, 09:40 am

Na Musa Mtepa

Mkurugenzi wa NGOs inayojihusisha na watun wenye ulemavu, Picha na Amua Rushita

Ulemavu ni hali ya kuwa na hitilafu ya  kudumu mwilini au akilini inayomzuia mtu kutekeleza shughuli zilizo kawaida katika maisha jamii, Ulemavu unaweza kuwa katika Mwonekano au aina tofauti kama vile viungo vya mwili miguu, mikono, mgongo  na viungo vingine vya mwili.

Nchini Tanzania katiba ya 1977 ilitambua haki za watu wenye ulemavu na kukataza aina zote za ubaguzi., Mnamo mwaka wa 2004, Wizara ya kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo ilitoa Sera ya Taifa ya watu wenye ulemavu, inayosisitiza kujitolea kwa wizara hiyo katika kuhakikisha kwamba kuna haki sawa kwa watu wenye ulemavu.

Nikukaribishe katika kipindi hiki ambapo hii leo tunaangazia Watu wenye ulevu na uanzishaji wa Asasi zinavyoweza kusaidia watu wenye ulemavu na changamoto wanazo kutana nazo.

Mwaandaaji na Msimuliaji wa Makala haya ni mimi Musa Mtepa wa Jamii fm Rdaio.