Sehemu ya mguu wa Ndg. Nogle
Jamii FM

Nipo tayari kukatwa mguu

4 February 2023, 14:29 pm

Ndg. Marias Thomas Ngole akiwa anaonyesha sehemu ya mguu ulio umia. PICHA na Musa Mtepa

“Wahisani na wadau wameombwa msaada wa matibu ya mguu kwa Ndg. Marias Thomas Ngole mkazi wa kitongoji cha Mijolo kijiji cha Ziwani Mkoani Mtwara baada ya kuapata ajali ya kugongwa na pikipiki miaka mitatu iliyopita.”

Na Musa Mtepa

Akizungumza na Jamii fm Radio jana Februari 3, 2023 Ndg. Marias amesema kuwa anachoomba ni msaada wa fedha au muhisani wa kwenda kumsaidia kumpeleka hospitali kutoa chuma au ikiwezekana hata kukata mguu wenyewe huku akielezea kuwa maumivu anayopitia ni makali kwani hata mfupa uliovunjika na kuungwa  umeshatolewa kwa njia ya kienyeji kutokana na mguu kuoza.

“hata kutembea siwezi hali inayo nipelekea haja ndogo na kubwa  kuitolea hapa hapa nilipokaa  huku  usingizi wangu kuupata ukiwa ni ndoto tangu miaka mitatu iliyopita” Amesema Marias.

“Hata kutembea siwezi hali inayo nipelekea haja ndogo na kubwa  kuitolea hapa hapa nilipokaa  huku  usingizi wangu kuupata ukiwa ni ndoto tangu miaka mitatu iliyopita”

Ndg. Juma  Musa Chinduli mwenyekiti wa kitongoji cha Mijolo amaethibitisha kuwepo kwa mgonjwa huyo Katika eneo lake na amewaomba watanzania kumsaidia kijana huyo anaye pitia mazingira magumu  kwani wao kama viongozi wamepamabana  kuhakikisha wanapata fedha za kumsaidia Bw Marias na imeshindikana  kutokana na hali ya kiuchumi ya wananchi  wa maeneo hayo.

Ndg. Marias Thomasi Ngole alipata ajali ya pikipiki Mwaka 2019 na kupata matibabu  ya kuwekwa chuma cha kuunga mfupa wa mguu uliovunjika katika hospitali ya Nyangao Mkoani Lindi  ambapo alipewa muda wa kurejea hospitalini hapo na alifanya hivyo ila kutokana na hali ya kiuchumi ya Bw Marias alishindwa kuipata fedha shilingi 200,000/= za kufanikisha kutoa chuma hicho.