Jamii FM

Tutawapa bima za afya; Kaimu mganga mkuu

15 May 2021, 19:43 pm

Na Karim Faida.

Kaimu Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Dkt Mathayo malaika amesema anashughulikia bima za afya za CHF kwa kaya moja masikini inayopatikana katika kijiji cha Namuhi kata ya Libobe Halmashauri ya wilaya ya Mtwara baada ya taarifa yao kuibuliwa na Jamii fm radio walipowatembelea nyumbani kwao na kuwakuta wakiwa na maisha magumu.

Kaimu Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Dkt Mathayo malaika

kupatikana kwa kadi hizo itawasaidia kupata tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya hata wasipokuwa na pesa

Amesema Dkt Malaika

Jamii fm radio ilipokea taarifa ya uwepo wa Mabibi wawili ambao ni Bibi Maimu Mkopoka na mdogo wake Somoe Mkopoka ambao wote wanaumwa mmoja TB na mwingine ameparalaizi, na wanaishi maisha magumu huku wakimtegemea mjukuu wao ambae anategemea kulima vibarua ndio awasaidie bibi zake.

Bibi Maimu Mkopoka na mdogo wake Somoe Mkopoka

Akiongea na Jamii fm radio Mwenyekiti wa kijiji hicho Ndugu Mohamedi Kuyaula alisema pamoja na mahitaji mengine wanayohitaji Mabibi hao, ni muhimu wangepatiwa bima ya afya kitu ambacho tayari serikali kupitia Kaimu Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara wanalishughulikia.

Makazi yao ya sasa