Jamii FM

Matukio ya mauaji yanaichafua Mtwara

5 May 2021, 20:49 pm

Na karim Faida

Diwani wa kata ya Mkunwa halmashauri ya wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara amesema katika kata yake imekuwa na Matukio ya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na mauaji ya watu watatu tofauti kwa matukio tofauti katika kipindi cha miezi mitatu yaani kuanzia Januari hadi Machi.

Diwani wa kata ya Mkunwa Mh Ismaili Mbwenga

Akiongea na Jamii fm radio leo baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Sabodo halmashauri ya wilaya ya Mtwara Diwani huyo amesema tayari wana mipango ya dhati ya kutokomeza hali hiyo kwa kuanzisha vikundi vya polisi jamii kwa ajili ya kulinda amani.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Mh Selemani Nampanye

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mtwara Mh Selemani Nampanye amewataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwa inatengeneza uhasama baina ya familia moja na nyingine na pia kurudisha nyuma maendeleo ya watu.

Ameongeza kuwa kama halmashauri watajenga kituo cha polisi mahususi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na amani katika kata hiyo ya Mkunwa ambayo pia ndio makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.