Jamii FM

Redio mara zote zinatoa habari za uhakika – Sharifu Kasimu

13 February 2024, 12:01 pm

Sharifu Kasimu Namkanda mkazi wa kata ya Naliendele mkoani Mtwara. Picha na Msafiri kipila

Na Msafiri Kipila

Jamii FM Radio imepata nafasi ya kuzungumza na Sharifu Kasimu Namkanda mkazi wa kata ya Naliendele mkoani Mtwara, ambaye anaeleza kuwa redio ina umuhimu mkubwa sana kwa jamii hasa kwa watu waliopo vijijini ambako mitandao ya kijamii na runinga inakuwa changamoto kufikika lakini pia hata mjini redio husikilizwa kwa wingi kwa kuwa redio ndicho chombo kinachosikikizwa na watu wengi.

Lakini pia ameendelea kusema kuwa redio mara zote zinatoa habari za uhakika na ndiyo maana itabaki kuwa chombo muhimu sana hata kama kumekuwa na wingi wa mitandao ya kijamii bado hii haiwezi kuathiri uwepo wa redio.

Akizungumza na Jamii FM bado amesisistiza kuwa upatikanaji wa habari kwa njia ya mtandao kumekuwa na changamoto kutokana na uwepo wa habari zenye upotofu tofauti na redio kwasababu waandishi wake wako makini na wanatangaza kile ambacho wamekitafuta wenyewe.

Sauti ya Sharifu Kasimu Namkanda Mkazi wa kata ya Naliendele mkoani Mtwara