Jamii FM

CUF yazindua kampeni uchaguzi serikali za mitaa Mtwara Mjini

21 November 2024, 22:26 pm

Makamu mwenyekiti wa CUF Tanzania bara Maftaha Nachuma akizindua kampenzi za uchaguzi wa serikali za mitaa (Picha na Musa Mtepa)

Huu ni uzinduzi wa kampeni kupitia chama cha Wananch CUF ikiwa ni ishara ya kutangaza sera na mweleko wa chama kwa wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika November 27,2024 kote nchini.

Na Musa Mtepa

Chama cha Wananchi CUF leo, Novemba 21, 2024, kimefanya uzinduzi wa kampeni zake kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Uzinduzi huo ulifanyika katika mtaa wa Magomeni viwanja vya Soko Bati, Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Katika hotuba yake, Makamu Mwenyekiti wa CUF Tanzania Bara, Maftaha Nachuma, amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi na kuwachagua viongozi wa CUF ili kuweza kutekeleza mikakati ya haki sawa kwa wote na sera ya utajirisho.

Sauti ya Maftaha Nachuma makamu mwenyekiti CUF Tanzania Bara.

Nachuma amesema kuwa sera ya utajirisho inakusudia kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuwapa fursa ya kutumia rasilimali za taifa, kama vile gesi, na hivyo kuchochea maendeleo ya vijiji na vitongoji.

Aidha amesisitiza kuwa, wananchi wanapaswa kutoa kura ya ndio kwa wagombea wa CUF ili kusaidia kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya uchumi na maisha ya kila siku ya wananchi.

Sauti ya Maftaha Nachuma makamu mwenyekiti CUF Tanzania Bara.

Kwa upande mwingine, Katibu wa CUF Mtwara Mjini, Saidi Kulaga, ameiomba taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mtwara kuchunguza na kutoa taarifa kuhusu tukio la aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti Mtaa wa Tandika kupitia CUF, ambaye amehama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo Kulaga amesema kuwa mgombea huyo amekiuka kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa, ambazo zinataka mtu kujitoa kwa utaratibu maalum.

Sauti ya 1 Saidi Kulaga katibu wa CUF Mtwara Mjini

Aidha, Kulaga amewasihi wananchi kuendelea kupigania mabadiliko katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Sauti ya 1 Saidi Kulaga katibu wa CUF Mtwara Mjini

Mwanachama wa CUF, Amina Liposwe, amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi bora na kusisitiza kuwa mamlaka ya kusimamia uchaguzi inapaswa kutangaza matokeo kwa haki, bila upendeleo.

Sauti ya Amina Liposwe Mwanachama wa CUF Mtwara Mjini.