Jamii FM

Zao la mwani Mtwara ladoda, wakulima walilia soko

11 October 2023, 14:34 pm

Mmoja wa wakulima wa mwani akionesha zao hilo ambalo bado amehifadhi nyumbani wakati akisubiri mnunuzi. Picha na Musa Mtepa

Zao la mwani limekuwa zao jipya katika mkoa wa Mtwara ambapo wanawake wanaoishi kata ya Msangamkuu wamechangamkia fursa hiyo ya kilimo cha mwani na sasa hawana soko la kuuza zao hilo.

Na Musa Mtepa

Wakulima wa zao la mwani wa kijiji cha Msangamkuu, kata ya Msangamkuu mkoani Mtwara wameiomba serikali kuwatafutia soko la uhakika la zao hilo ili waweze kupata tija ukilinganisha na hali ya soko lake kwa kipindi hiki.

Wakulima wa zao la Mwani wakika katika kikao kwenye kata ya Msangamkuu: Picha na Musa Mtepa

Wakizungumza na Jamii FM Radio wakulima hao wamesema kuwa zao la mwani limekuwa na  changamoto kubwa kwenye uzalishaji wake kuanzia hatua za awali hadi kufikisha sokoni hivyo serikali  na wadau wa maendeleo hawana budi kuwatafutia masoko ya uhakika wa zao hilo walilohamasika kulima kwa wingi kwa wananchi wa kata ya Msangamkuu.

Sauti za wakulima mbalimbali wa Mwani Mkoani Mtwara

Naye diwani wa kata hiyo Mheshimiwa Hamisi Saidi Mangorosho amekiri kuwepo kwa changamoto ya soko kwa wakulima hao huku akiahidi kufanyia kazi kwa kwenda kuzungumza na afisa biashara na mkurugenzi wa halmashauri ili kuhakikisha linapatikana soko la uhakika.

Sauti ya Diwani wa kata ya Msangamkuu Ndugu Hamisi Saidi Mangorosho

Akitoa mafunzo ya kulipa thamani zao hilo mwenyekiti wa mtandao wilaya na mjumbe wa kamati tendaji TUNA ALIENCE  Shabani Mayonzi amesema kuwa ili kuondoa changamoto zote wanazokutana nazo wakulima hao ni lazima watengeneze vikundi vya wakulima wa mwani ili kutengeneza umoja utakaosaidia kupata soko la uhakika na kuongeza tija kwa wakulima hao.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtandao wa TUNA ALIENCE – Ndugu Shabani Mayonzi