Jamii FM

Ukidhulumiwa Ardhi, fuata utaratibu

28 June 2021, 15:44 pm

Na Karim Faida

Wananchi wametakiwa kuwatumia watu sahihi pale panapotokea migogoro ya ardhi ili kupata majibu sahihi hatua ambayo itasaidia kuondokana na migogoro inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Wakili Amani Mkwama

Hayo yamesemwa na Wakili Amani Mkwama katika mafunzo ya Waandishi wa habari yanayohusu haki za binadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha msaada wa Kisheria na haki za binadam Tanzania LHRC yanayoendelea mkoani Morogoro kwa siku tatu mfululizo.

waandishi wa Habari katika mafunzo yaliyoandaliwa na LHRC

Waandishi hao wa habari kutoka mikoa minne Tanzania wamekili kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi katika maeneo yao na kupitia mafunzo hayo wameahidi kuibua na kutangaza migogoro mbalimbali ya ardhi ili kutoa elimu kwa wasio na utambuzi hasa wale waliopo vijijini.