Jamii FM

Masasi wajadili maendeleo ya Wilaya

10 January 2021, 16:16 pm

Wajumbe wa kamati ya ushauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara

KIKAO cha Kamati ya Ushauri Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ( DCC) jana tarehe 9, 2021 kimeketi kwa ajili kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha, 2020/ 2021 ikiwa ni kikao cha kwanza kwa mwaka 2021

Aidha, Wajumbe wa kikao hicho wakiongozwa na mwenyikiti wa kikao hicho ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee wamepitisha maazimio mbalimbali juu ya masuala yaliyojadiliwa na wajumbe wa kikao, ikiwemo kuzitaka taasisi za fedha Wilayani humo kutoa elimu ya mikopo ya ujenzi wa nyumba kwa wananchi, upatikanaji ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na ardhi.

Wajumbe walioudhulia katika kikao hicho ni watendaji wa Halmashauri zote mbili ile ya Mji Masasi na wilaya ya Masasi, viongozi wa dini, vyama vya siasa, wazee maarufu na Asasi zisizo za kiserikali, kikao hicho kimefanyika mjini Masasi katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri ya wilaya Masasi.