Jamii FM

Makala: Uhamasishaji wa kutunza bahari kwa manufaa ya baadae

18 February 2023, 09:24 am

Miti aina ya mikoko inayohifadhi mazingira ya bahari. Picha na Musa Mtepa

By Musa Mtepa

Ni mkala inayohusisha tasisi ya kiraia ya jumuia ya umoja wa wavuvi wa Jodari nchini Tanzania maarufu TUNA ALLIANCE ambao walifanya utafiti wa mazingira ya Bahari ya Hindi kutoka visiwani Zanzibar hadi mikoa ya Lindi na Mtwara.

Wakati wa utafiti wao wamegundua kuwa bahari na pwani ya kusini imeharibiwa kutokana na shughuli za uvuvi hivyo, jumuia hiyo wakaanza kutoa mafunzo kwa watumiaji wa bahari hususani wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kuwapa elimu juu ya uvuvi bora, utunzaji wa bahari kwa kupanda miti aina ya mikoko na athari za kuharibu uoto wa asili wa bahari.