Mwenyekiti wa kijiji cha Madimba Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ndugu Dominick Namavanga akizungumza na Musa Mtepa wa Jamii FM Radio
Jamii FM

Fahamu manufaa ya uwepo wa shughuli za Gesi Kijiji cha madimba katika Miradi ya Maendeleo – Makala

5 February 2024, 14:08 pm

Mwenyekiti wa kijiji cha Madimba Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ndugu Dominick Namavanga akizungumza na Musa Mtepa wa Jamii FM Radio
Mwenyekiti wa kijiji cha Madimba Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ndugu Dominick Namavanga akizungumza na Musa Mtepa wa Jamii FM Radio

Kwa mujibu wa SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema kiwango cha uchakataji wa gesi asilia kwa miaka nane katika kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba   kimeongezeka kutoka futi za ujazo milioni 20 mwaka 2015 hadi kufikia futi za ujazo milioni 110 mwaka 2023

Na Musa Mtepa

Mkoa wa Mtwara ni mkoa uliobarikiwa kuwa na Rasilimali mbalimbali zinazojitambulisha kitaifa na  kimataifa.

Rasilimali hizo ni pamoja  na Kilimo cha zao la Korosho na  uwepo wa Gesi Asilia Mkoa umekuwa ukitambulishwa kitaifa na kimataifa .

Gesi Asilia ambayo imekuwa utambulisho mkubwa kwa Mikoa  ya kusini Lindi na Mtwara ambapo kwa mkoa wa Lindi 1974 iligunduliwa Songosongo Wilayani Kilwa na Mtwara ni 1982 katika eneo la MnaziBay  kata ya Msimbati Halmashauri ya Mtwara Vijijini Mkoani Mtwara  ambapo shughuli Rasmi za uchimbaji na uchakataji ulianza mwaka 2014 katika kijiji cha Madimba kilomita chache kutoka chanzo cha Nishati hiyo

Nikukuaribishe katika kipindi hiki cha Gesi na Mazingira ambapo hii leo tunaangazia uwepo wa shughuli za  gesi asilia  unavyowanufaisha  wananchi wa madimba kupitia miradi ya maendeleo.

Mwandaaji na Msimuliaji wa kipindi hiki ni mimi MUSA MTEPA Wa Jamii fm Radio.

Kusikiliza makala haya Bonyeza hapa