Jamii FM

Jamii yatakiwa kufahamu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji

18 April 2024, 21:57 pm

Mkulima wa mpunga akifanya shughuli za kilimo kwenye vyanzo vya maji moja ya Bwawa linalopatikana katika mkoa wa Mtwara (pich na Msafiri Kipila)

Shughuli zinazofanywa karibu na vyanzo vya maji zimekuwa zikihatarisha uwepo wake huku mamlaka zikiombwa kuendelea kutoa elimu ya athari hasi na umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji.

Na Msafiri Kipila

Mammlaka zinazo simamia vyanzo vya maji zimeombwa kutoa Elimu kwa wananchi juu ya athari hasi na umuhimu wa utunzaji wake ili kuepuka kuharibiwa kunakotokana na ongezeko la mahitaji na  iadadi ya Watu.

Wakizungumza na Jamii fm radio  16/4/2024 baadhi ya Wananchi wa kata ya Mtawanya Manispaa ya Mtawara Mikindani wamesema kuwa ili kuepuka uharibifu wa vyanzo vya maji mamlaka na idara husika wanatakiwa kushirikiana na serikali za mitaa ili kurahisha kufikisha elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji kwa njia rahisi.

 Sharifu Kassimu Namkanda  mkazi wa mtaa wa Mtawanya Manispaa ya Mtwara Mikindani amesema vyanzo vya vilivyopo ni vya muda mrefu hivyo uhitaji wake ni mkubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo watu walikuwa wachache.

Sauti ya Sharifu Namkanada mkazi wa mtaa wa Mtawanya Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Akizungumzia Uelewa wa Wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji mkuu wa kitengo cha uhamasishaji   kutoka ofisi ya bodi ya maji bonde la Ruvuma na pwani ya kusini Bw Dicksoni Maganga amesema kuna baadhi ya wananchi wanaamini kuwa maji ni rasilimali ambayo inayotoka kwa Mungu  hali inayowafanya kutowajibika katika utunzaji wa vyanzo hivyo.

Sauti ya Dickson Maganga mkuu wa kitengo cha uhamasishaji   kutoka ofisi ya bodi ya maji bonde la Ruvuma na pwani

Aidha naye Bonifasi Msemwa mkuu wa kitengo cha utunzaji bonde kutoka ofisi ya bodi ya maji bonde la ruvuma na pwani ya kusini ameitaka jamii kuhakikisha inatunza vyanzo vya maji kwa kutofanya shughuli yeyote hatarishi katika eneo la chanzo .

Sauti ya Bonifasi Msemwa mkuu wa kitengo cha utunzaji bonde kutoka ofisi ya bodi ya maji bonde la Ruvuma na pwani.