Serikali yatakiwa kuwa na mipango endelevu matumizi ya gesi asilia
9 September 2024, 21:48 pm
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilikuwa katika ziara ya kakizi katika kujionea miradi mbalimbali ya inayotekelezwa katika jamii kupitia urejeshwaji wa jamii (CSR) kuptia Shirika la Maendeleo ya Petrol Nchini TPDC katika vjiji vya Msimbati,Mngoji na Madiba ambapo miradi kama kituo cha Afya,Kituo cha Polisi na Taa za Barabarani imeanza kutekelezwa.
Na Musa Mtepa
Kamati ya kudumu ya Bunge ya nishati na Madini imeishauri serikali kuwa na mipango endelevu ya matumizi ya Gesi asilia inayozalishwa nchini kwa kukuwa jamii inauelewa umuhimu wa matumizi ya nishati hiyo.
Akizungumza leo September 9, 2024 Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya nishati na Madini Kilumbe Ng’enda amesema Watanzania wengi wameanza kuelewa manufaa ya gesi asilia katika kupikia,kuendeshea magari hivyo ni wakati wa kuongeza kasi ya uzalishaji ,usambazaji na ushirikishaji wa wadau kwenye vituo vya kuuza gesi kwa ajili ya Magari.
Aidha Mh: Kilumbe meitaka serikali kuipa umuhimu wa Barabara inayotokea mjini kuelekea Msimbati kutengenezwa kwa kiwango cha Lami kwa manufaa ya Wananchi Pamoja na viongozi wanaotembelea katika maeneo hayo
Kwa uapnde wake Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema kuwa wao kama serikali wamepokea maelekezo yaliyotolewa huku akiishukuru kamati hiyo kwa kuridhishwa na miradi inayotekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini(TPDC) hususani ya CSR ikiwemo mradi wa kituo cha Afya Msimbati,kituo cha Polisi na mradi wa taa Barabarani iliyowekwa katika vijiji vya Msimbati,Mngoji na Madimba.
Akizungumzia ujio wa kamati hiyo Meneja mkuu wa kampuni ya GASCO Mhandisi Baltazar Thomas amesema kuwa kamati ilikuja kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya urejeshwaji wa jamii (CSR) huku akizungumzia kiwango cha Gesi kinachozalishwa kwa hivi sasa katika eneo la uchakatwaji wa gesi asilia.