Rais Samia kufanya ziara ya siku 4 Mtwara
9 September 2023, 17:01 pm
Hii ni Mara ya kwanza kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kufanya ziara mkoani Mtwara akiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo kwa mara ya mwisho alifanya mwaka 2016 akiwa Makamu wa Rais.
Na Musa Mtepa
Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani anatarajia kufanya ziara ya siku nne mkoani Mtwara kuanzia September 14 mpaka September 17, 2023.
Akizungumza na Waandishi Habari leo ofisini kwake September 9, 2023 Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanal Ahmedi Abbas amesema kuwa pamoja na mambo mengine Rais anatarajia kufanya ufuatiliaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) pamoja na kutembelea utekelezaji wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa mkoani Mtwara.
Aidha Kanal Ahmedi Abbas amewaomba wananchi kujitokeza kumlaki kwa wingi katika maeneo yote atakayopita na kuhudhuria mikutano atakayohutubia akiwa mkoani Mtwara.
Hii ni Mara ya kwanza kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kufanya ziara mkoani Mtwara akiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo kwa mara ya mwisho alifanya mwaka 2016 akiwa Makamu wa Rais.