Jamii FM

RC Kanali Sawala aitaka jamii ya Mtwara kuliombea Amani Taifa

6 April 2024, 20:58 pm

 Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanal Patrick Sawala akitoa neno la shukrani kwa hadhira iliyojitokeza kufuturu hapo jana(Picha na Mtwara rs)

Binadamu hakuna aliyekamilika  mmoja anaweza kumkosea mwingine kwa bahati mbaya bila kutambua hivyo tuendelee kusameheana

Na Musa Mtepa

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amewataka Wananchi kuendelea kuliombea amani taifa pamoja na kusameheana pale inapotokea kukoseana ili kuendelea kuwa na mshikamano na upendo uliopo hivi sasa .

Wito huo ameutoa Jana 5/4/2024 Kwenye hafla ya Iftari iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa ambapo amesema kuwa Binadamu hakuna aliyekamilika  mmoja anaweza kumkosea mwingine kwa bahati mbaya bila kutambua hivyo tuendelee kusameheane ili Mtwara iendelee kuwa na mshikamano na amani na kimbilio la watu wengine.

Sauti ya Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara

Naye aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilethuri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ambae pia ni Katibu wa kamati ya Amani mkoa wa Mtwara  Lucus Mbedule ameitaka jamii kuendelea kuishi katika misingi ya tabia ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Sauti ya Askofu Lucus Mbedule katibu wa kamati ya Amani mkoa wa Mtwara

Akizungumza kwa niaba ya Wenyeviti wa Halmashauri zote 9 za mkoa wa Mtwara Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Baisa Abdala Baisa amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kitendo cha kuwajumuisha na  kuwafuturisha pamoja,huku akuimbusha jamii ya Wanamtwara kuwa na utaratibu wa kutoa Sadaka kama Mtume Muhammadi (S.W.A) alivyohimiza kutenda mambo mema na kutoa sadaka.

Sauti ya Baisa Abdala Baisa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba