

16 April 2025, 14:06 pm
Makala hii inalenga kuhamasisha jamii kuhusu haki ya watu wenye ulemavu kupata elimu na kutumia teknolojia saidizi kwa maendeleo yao binafsi na ya jamii kwa ujumla. Kupitia mfano wa Mwalimu Shazili Ali Namangupa wa Shule ya Msingi Nanguruwe, inaonyesha jinsi elimu jumuishi na teknolojia kama fimbo nyeupe na simu janja zinavyoweza kubadili maisha ya walimu na wanafunzi wasioona.
Na Msafiri Kipila
Katika juhudi za kuleta maendeleo jumuishi kwa jamii, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya utoaji elimu kwa watu wenye ulemavu. Shule ya Msingi Nanguruwe, iliyopo kata ya nanguruwe katika mkoa wa Mtwara, sasa inatoa elimu kwa wanafunzi wasioona, jambo ambalo awali halikuwepo.
Shazili Ali Namangupa, mwalimu katika shule hiyo, anasema mabadiliko hayo ni hatua kubwa katika kujenga jamii inayojali usawa na fursa kwa wote. “Unapompatia mtoto mwenye ulemavu elimu, unabadilisha mtazamo wa jamii na kuondoa dhana ya kuwafungia ndani watoto hao bila kuwapa fursa ya kusoma,” anasema Mwalimu Shazili.
Kupitia mafunzo maalum ya teknolojia saidizi, ikiwemo matumizi ya fimbo nyeupe na baadaye simu janja, Mwalimu Shazili ameweza kuboresha utendaji wake wa kazi. Anaeleza kuwa teknolojia imemsaidia sana kurahisisha majukumu yake ya kila siku.
Sikiliza Makala haya juu ya watu wenye ulemavu