TAKUKURU Mtwara yawanoa wanahabari uchaguzi serikali za mitaa
11 November 2024, 18:04 pm
Haya ni mafunzo yenye lengo la kuwawezesha waandishi wa Habari mkoani Mtwara kutambua kanuni na taratibu zitakazo waongoza katika ufanyaji kazi katika kuelekea uchaguzi wa serika za mitaa November 27,2024
Na Musa Mtepa
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) Mkoa wa Mtwara leo November 11, 2024 imefanya mafunzo kwa waandishi wa Habari juu ya elimu inayohusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika November 27, 2024 kote nchini.
Akizungumzia lengo la mafunzo hayo naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Jumbe Makoba amesema lengo ni kuwapa elimu inayohusu uwelewa wa kanuni,miongozo na taratibu zilizopo kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wakijua wapo ndani ya mipaka kupitia mafunzo waliyopewa.
Aidha Bw Makoba amesema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia katika kuibua na kutangaza vitendo vyenye viashiria ya Rushwa aidha kwa wagombea au Wananchi na hatua ziweze kuchukuliwa.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambae pia Mjumbe wa uchaguzi wa kamati ya uchaguzi ngazi ya mkoa wa Mtwara Bw Hassani Linyama amesema mafunzo hayo yamekuwa muhimu kwa Waandishi wa Habari ili kuweza kupata uelewa juu ya yale yanaendelea katika jamii.
Nao Waandishi wa Habari wameonesha kufurahishwa na mafuzno hayo kwakuwa yatawasaidia katika utendaji kazi wao kwa kufuata kanuni na taratibu zilizopo katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za TAKUKURU katika kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanatambuakanuni,taratibu pamoja na kuibua viashiria vya vitendo vya Rushwa katika uchaguzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.