Jamii FM

Serikali yatumia zaidi ya Sh Milioni 560 kujenga Shule ya Sekondari Chikota

12 August 2026, 16:51

Jengo la utawala la shule ya sekondari Chikota iliyopo katika halmashauri ya mji Masasi yenye zaidi ya thamani Milioni 560(Picha na Musa Mtepa)

Serikali imetumia zaidi ya Sh milioni 560.52 kujenga Shule ya Sekondari Chikota, Halmashauri ya Mji Nanyamba, Mtwara, huku Serikali ikiahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili shule hiyo

Na Musa Mtepa

Serikali imewezesha ujenzi wa Shule ya Sekondari Chikota katika Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni 560.52.

Kati ya fedha hizo, Sh milioni 471.4 zimetumika katika ununuzi wa vifaa vya ujenzi, huku Sh milioni 89.4 zikitumika kulipia mafundi waliotekeleza ujenzi huo.

Hayo yamesemwa leo, Agosti 12, 2026, na Mkuu wa Shule ya Sekondari Chikota, Mwalimu George Danford, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo uliojengwa katika Halmashauri ya Mji Nanyamba.

Sauti ya 1: George Danford, Mkuu wa Shule

Aidha, Mwalimu Danford amesema awamu ya kwanza ya mradi huo imekamilika, huku miundombinu yote iliyopangwa katika awamu hiyo ikiwa imejengwa.

Sauti ya 2: George Danford, Mkuu wa Shule

Kwa upande wake, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Michael Mtenjele, amewataka wananchi, walimu na wanafunzi kutunza miundombinu ya shule hiyo ili Serikali iweze kuendelea kuboresha na kujenga miundombinu mingine katika shule hiyo na maeneo mengine nchini.

Sauti ya 3: Kanali Michael Mtenjele, Mkuu wa Wilaya

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema kwa kushirikiana na Waziri wa Elimu atazifanyia kazi changamoto zinazoikabili shule hiyo, ili kuwezesha wanafunzi kupata mazingira bora ya kujifunzia na elimu yenye ubora.

Sauti ya 4: Judith Kapinga, Waziri wa Viwanda na Biashara

Aidha, Waziri Kapinga amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi wa Serikali, hususan pale wanapokutana na changamoto, kwa kuwafikishia taarifa na changamoto hizo kwa wakati, ili Serikali iweze kuzifanyia kazi na kuendelea kupeleka miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Sauti ya 5: Judith Kapinga, Waziri wa Viwanda na Biashara