Jamii FM

Waziri Kapinga aweka jiwe la msingi shule ya msingi Chilimba-Masasi

12 August 2026, 00:12

Mwonekano wa jengo la utawala shule ya msingi Chilimba wilayani Masasi (Picha na Musa Mtepa)

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, ameweka jiwe la msingi katika Shule ya Msingi Chilimba, Masasi, na kuwataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Na Musa Mtepa

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, leo Agosti 11, 2026, ametembelea na kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Msingi Chilimba, iliyopo katika Kijiji cha Chilimba, Kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe hilo la msingi, Mhe. Kapinga amewataka wananchi wa Chilimba kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Sita, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi katika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

SAUTI YA 1: JUDITH KAPINGA – WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA

Aidha, Waziri Kapinga amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo, huku akimtaka kuendelea kusimamia na kukamilisha kwa wakati miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa kwa ajili ya wananchi.


SAUTI YA 2: JUDITH KAPINGA – WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA

Akitoa taarifa kuhusu Shule ya Msingi Chilimba, iliyokuwa imeanzishwa mwaka 1930, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mateso Issack Bakari, amesema Serikali kupitia miradi ya BOOST imetoa zaidi ya shilingi milioni 409 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi yenye mkondo mmoja, hatua inayolenga kukabiliana na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya shule hiyo.


SAUTI YA 3: MATESO ISSACK BAKARI – MWALIMU MKUU

Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Chilimba wameipongeza Serikali kwa hatua ya kuijenga upya shule hiyo, wakieleza kuwa uchakavu wa miundombinu ya awali ulikuwa ukiathiri mazingira ya kujifunzia kwa watoto wao.

SAUTI YA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHILIMBA, MASASI